Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Monday 28 January 2013

MAHAKAMA YA KISUTU YAMPA DHAMANA LULU

 
MAHAKAMA KUU YAMPA DHAMANA MSANII MAARUFU LULU KUTOKANA NA KESI YAKE YA MAUAJI YA MSANII MWENZAKE KANUMBA

MSANII maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata dhamana leo baada ya kukidhi masharti ya dhamana aliyowekewa na mahakama.

Dhamana hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya hoja za mawakili wanaomtetea kukubalika.

Masharti aliyokuwa amepewa ni pamoja na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali wenye kiasi cha Sh. milioni 20 kila mmoja na kuwasilisha pasi ya kusafiri ya msanii ili kutotoka nje ya nchi hadi kesi hiyo itakapokamilika.

Huku mashabiki wake na baadhi ya wasanii wenzake wakiwa na furaha mahakamani hapo, kila mmoja alisikika akisema Mungu mkubwa.

Msanii Lulu akishuka katika Karandinga la Magereza wakati akipelekwa mahakamani Kisutu siku nyuma kwenda kusikiliza mwenendo wa kesi yake

Elizabeth Michael ‘Lulu’ akisubiri dhamana mahakamani.


No comments:

Post a Comment