Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Wednesday 30 January 2013

CHANGAMOTO YA KUWA NA MAKAZI BINAFSI

SEHEMU YA KWANZA
Watanzania wengi wamejenga makazi yao ya kudumu kwa namna ambayo hata ukielezwa huwezi kuamini kuwa mtu wa kawaida anaweza kujenga. Uzoefu unaonesha kuwa, ujenzi wa nyumba hufanyika kwa kupata mkopo toka benki, mahali pa kazi au kwa kwa mtu yeyote mwingine mwenye pata kubwa.

Mishahara ya wafanyakazi walio wengi ni aghalabu kumudu gharama za ujenzi wa nyumba. Kwa mara nyingi mishahara hiyo ni midogo sana. Ukiangalia tu kima cha chini cha mshahara ni kweli kabisa mtu hawezi kununua kiwanja au kujenga nyumba. 

Mathalani, thamani ya kiwanja kilichopimwa na serikali ni kubwa mno, achilia mbali viwanja ambavyo vinauzwa na watu binafsi. Ukigusa kiwanja unaambiwa mamilioni ya pesa. Kwa wengi wetu tumekata kabisa tamaa ya kuendelea kutafuta viwanjwa au kufikiria kununua viwanja. Unajiuliza, kula tu ni kwa shinda, kweli nitamudu kununua kiwanja na kujenga?

Kila mmoja wetu hujiuliza. Binafsi nimepatwa na changamoto kubwa katika kufikiria hatua ya kufikiria kuwa na kiwanja changu, na pengine kuwa na nyumba kabisa. Kwa jamii ya Kitanzania ambayo kwa kiwango kikubwa imegubikwa na umaskini wa kupindukia, wanajitahidi kupambana ili angalau waweze kupata mahali pa kudumu pa kuishi. Mchakato wa kutafuta kiwanja hadi kujenga huchukua miaka kadhaa kuanzia miaka mitano hadi kumi na pengine kuzidi kumi. Inategemea aina ya shughuli ambayo inamwingizia kipata mtu yule. 

Kwa sasa kuna mambo mengi ambayo yanawanya watu kuyafikiria katika mchakato wa ujenzi au ununuzi wa viwanja. Mmojawapo ni kujiunga na vikundi vya mikopo. Wapo wengine ambao hufikiria dili au safari za kikazi ambapo wana fursa ya kupata kipata kikubwa kidogo ambacho mara nyingi huwa nje ya bajeti. 

Sehemu ijayo, nitaendelea kuelezea changamoto mbalimbali ambazo zinawapata wananchi wa kawaida (maskini katika kutafututa viwanja na kujenga; pia tutaangalia hatari ya mwongezeko wa msongamano katika makazi haya mapya).







































































No comments:

Post a Comment