Jinsi ya kujua kama Uzito wako unaendana na Kimo chako
kiafya
By Dr. Joachim Mabula - On Jan 19th
2013 - in Afya
BMI hupatikana kwa kugawanya Uzito
(Weight in Kg) kwa (Kimo mara Kimo) (Kimo/Height in M) au Uzito (Weight in Kg)
gawanya kwa (Kimo mara Kimo) (Kimo/Height in Cm). Jibu utakalopata, zidisha kwa
10,000 au Uzito (Weight in Lb) gawanya kwa (Kimo Mara Kimo) (Kimo/Height in In)
na Jibu utakalopata zidisha kwa 703.
Body
Mass Index (BMI) ni njia nzuri na kuangalia kama Uzito wako upo katika afya
njema.
Kwa
watu wazima, BMI ni Kipimo cha kujua kama Uzito wako unaendana ka kimo chako.
Kwa
watoto wa Umri wa Miaka miwili na zaidi, BMI Centile hutumika. Hiki ni Kipimo
cha kujua kama Uzito wa Mtoto unaendana Na Kimo, Umri na Jinsia.
BMI
hupatikana kwa kugawanya Uzito (Weight in Kg) kwa (Kimo mara Kimo) (Kimo/Height
in M) au Uzito (Weight in Kg) gawanya kwa (Kimo mara Kimo) (Kimo/Height in Cm).
Jibu utakalopata, zidisha kwa 10,000 au Uzito (Weight in Lb) gawanya kwa (Kimo
Mara Kimo) (Kimo/Height in In) na Jibu utakalopata zidisha kwa 703.
Ukiwa na BMI inayozidi mipaka, upo katika
hatari zaidi ya Matatizo ya kiafya kama Kisukari aina ya Pili (Type II
Diabetes), Ugonjwa wa Moyo (Heart Disease) na Saratani (Kansa) za aina tofauti
tofauti.
Baadhi ya watu wazima wana maumbo
makubwa yanayoweza kusababisha BMI iwe juu zaidi ya mipaka; Mfano wachezaji wa
Rugby ambao wanaweza kuwa na Uzito uliozidi sana (Obese BMI) ingawa wana miili
midogo. Hata hivyo, hii haitaweza kutumika kwa watu wote.
BMI KWA WATU WAZIMA (BMI FOR
ADULTS):
BMI inazingatia kuwa watu wako na
maumbo na ukubwa tofauti tofauti. Ndio maana mipaka (Range) ya BMI inaonyesha
ni ya afya njema kwa watu wazima wa kila kimo.
BMI zaidi ya mipaka ya Afya Njema,
huonyesha kwamba una Uzito unaozidi kimo chako.
Mipaka ifuatayo hutumika kwa watu
wazima tu:
BMI chini ya 18.5: Huonyesha kwamba
upo chini ya Uzito (Underweight).
BMI kati ya 18.5 na 24.9: Huonyesha
mipaka ya afya njema. Huonyesha kuwa uzito wako unaendana na kimo chako kiafya.
BMI kati ya 25.0 na 29.9: Huonyesha
kuwa hali imezidi mipaka ya kawaida, hali inayomaanisha Uzito wako umezidi
kawaida (Overweight). Pia inamaanisha kuwa wewe ni mzito zaidi kuliko mtu
mwenye afya njema wa kimo chako.
Uzito uliopita kawaida unakuweka
katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo, kupooza (Stroke) na kisukari aina ya
pili (Type II Diabetes).
BMI ya 30 na zaidi: Inachanganuliwa
kama uzito kupita kiasi (Obese). Kuwa na Uzito kupita kiasi (Obese) kunakuweka
katika hatari zaidi ya Matatizo ya Kiafya kama Ugonjwa wa Moyo, Kupooza
(Stroke) na Kisukari aina ya Pili (Type 2 Diabetes).
Kupunguza Uzito kuna faida nyingi
ikiwa ni pamoja na kuleta kuimarika kwa afya, kuondoa maumivu ya mgongo na
viungo.
Funguo
kubwa za kupunguza uzito ni kupunguza vyakula vya wanga (Meals with Calories)
na kufanya mazoezi ya mwili.
Kiwango cha Mazoezi ya Mwili
huendana na umri. Watu wazima wa kati ya Umri wa Miaka 18 hadi 64 wanapaswa
kufanya mazoezi kwa angalau dakika 150, Mazoezi kama kutembea kwa haraka na
kuendesha baiskeli.
Kwa watu wazima wenye Uzito uliozidi
kiasi, wanapaswa kufanya zaidi ya kutembea kwa haraka na kuendesha baiskeli.
CHATI
YA KIMO NA UZITO (HEIGHT AND WEIGHT CHART)
Unaweza
pia kutumia chati ya kimo na uzito ili kuweza kujua kama uzito wako unaendana
na kimo chako kiafya. Chati ya kimo na uzito ni chati flani inayowekwa ukutani
inakuwa urefu na uzito na hivyo mtu akipima uzito analinganisha na kwenye
chati.
BMI
KWA WATOTO (BMI FOR CHILDREN)
Kukokotoa
BMI kwa mtoto, wataalamu wa afya huangalia uzito wa mtoto kwa kimo, umri na
jinsia. Matokeo yake huitwa ‘BMI Centile’. BMI Centile ni njia nzuri kwa
wataalamu wa afya kutambua kama mtoto ana uzito mzuri kiafya na kujua kama
mtoto anakua kama inavyotegemewa.
BMI Centile hupatikana baada ya
kupata jibu kwenye BMI ya kawaida na kulilinganisha kwenye chati ya BMI ya
mtoto wako kulingana na jinsia yake; iwe ya kike au ya kiume, kuna chati yake
maalumu. Unaweza kuwa umeshawahi fanya hivyo kwenye kadi ya makuzi ya mtoto
wako.
Baada ya kukokotoa BMI Centile,
Mtoto huanguka kwenye moja kati ya makundi manne:-
Chini
ya Uzito (Under Weight): Chini ya BMI Centile ya Pili (Below 2nd BMI Centile).
Uzito
mzuri kiafya (Healthy Weight): Kati ya BMI Centile ya Pili na ya Tisini
(Between the 2nd & 90th BMI Centile).
Uzito Kuzidi (Overweight): Kati ya
BMI Centile ya Tisini na Moja na Tisini na Saba(Between 91th to 97th BMI
Centile).
Uzito kuzidi kiasi (Very
Overweight/Obese): BMI Centile ikiwa ya Tisini na Nane na zaidi.
Kama
mtoto wako ana Uzito uliozidi kiasi (Obese) atakuwa katika hatari ya kubwa ya
kuugua sana kipindi chake cha utoto hata katika maisha ya baadaye.
Endelea Kufuatana
nami kwa Makala zijazo, Nitakuelekeza jinsi ya kupunguza Uzito na uwe na afya
No comments:
Post a Comment