Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Wednesday 9 January 2013

UTAFITI WA KAUKI

KAUKI INAFANYA UTAFITIUmoja wa Ukoo wa Kivenule upo katika mchakato wa utafiti kuhusiana na chanzo, muundo na mgawanyiko wa Ukoo wa Kivenule, na pia mwingiliano na jamii zingine. Utafiti huu umechukua takribani miaka nane na bado unaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali.

Utafiti huu pia utaangalia Koo mbalimbali ambazo zimeingiliana na Ukoo wa Kivenule na pia Ukoo wa Kivenule ulivyoweza kuingia katika koo nyingine. Pia, utafiti utatathmini athari hasi na chanya za mwingiliano huu na pia uhusiano wa Koo mbalimbali katika himaya ya Uhehe.


Pia utafiti utagusa maeneo ya chimbuko la koo mbalimbali ndani ya uhehe, miiko na historia mbalimbali za koo zilizopo katika mkoa wa Iringa. Pia utaangalia uhusiano uliopo baina ya Kabila la Wahehe na Wabena.

Utafiti utaenda mbali zaidi na kuangalia mila na desturi za wahehe, aina za vyakula, tamaduni mbalimbali zinazotawala kabila hili na mengine mengi.

Angalia link hii yenye kurasa 75 za Muundo wa Ukoo wa Kivenule:http://attachments.wetpaintserv.us/HViFLxKQKO-q_cwQzFWieA764631

OMBI

KAUKI inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo zile za ukusanyaji taarifa sahihi, kumudu gharama za safari, malazi na kujikimu wakati wa kufanya kazi hii. Vile vile uhakiki wa taarifa umekuwa ukichukua muda mrefu kutokana na kukosa taarifa sasa hivi au vyanzo mbadala kutokana na wazee wengi kufariki na hivyo jamii kutokuwa na vyanzo mbadala vya taarifa. Pamoja na changamoto hii, tunatumia vyanzo mbalimbali vinavyopatikana ili kuweza kupata taarifa.


Kwa wadau wapenda tamaduni, desturi na pia historia ya Kabila la Wahehe, tunaomba mtuunge mkono kwa kila namna na pia ikibidi kutusaidia baadhi ya vitendea kazi ambavyo vitarahisisha kazi yetu. Pia watu wenye taarifa za kutosha, tunawaomba watuunge mkono kwa kutupatia taarifa hizo.

Tunatanguliza shukrani zetu.



Kwa anuani na mawasiliano,


Adam Kivenule (Mtafiti) kwa kushirikiana na Japo na Watafiti Wasaidizi (William Sigatambule Kivenule, Donath Peter Mhapa, Ignas Pangayena Kivenule na Innocent Samwel Kivenule).

E-mail: tagumtwa.kauki@gmail.com

           kivenule@gmail.com

+255 713 270364

No comments:

Post a Comment