TAARIFA
KWA UMMA WA WANA-KAUKI NA JAMII KWA UJUMLA
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 9
wa KAUKI, unaenda sambamba na kuangalia mafanikio na changamoto mbalimbali
ambazo KAUKI inaendelea kukumbana nazo. Lakini katika maisha yeyote ya
binadamu, mafanikio na changamoto huenda pamoja.
Mafanikio makubwa ambayo KAUKI
imeyapata kwa kipindi cha miaka 8 ni pamoja na:
- Kuwaunganisha Wanaukoo kutoka maeneo ya Kidamali, Nduli, Magubike, Igominyi, Nduli, Ilalasimba, Kalenga, Mufindi, Irore, Nyamahana, Mgongo, Nyamihuu, Idodi, Idete, Mufindi, Iringa Mjini, Itagutwa, Mtera, Morogoro, Kilombero, Dar es Salaam na Dodoma. Watu wengi wameweza kufahamiana tofauti na mwanzo.
- Kufahamiana baina yetu pia kumetufanya tujitambue na pia kuona athari ya kuingiliana majina kutokana na uwingi wetu. Ushirikiano umeanza kuonekana katika matukio mbalimbali ya Kijamii. Blogu yetu ya http://www.tagumtwa.blogoak.com imekuwa ni kiunganishi kikubwa kwa sababu taarifa mbalimbali zimeanza kusambazwa.
- Ushirikiano na upendo wa dhati baina yetu sasa umeanza kuonekana, na tunashirikiana katika shida na raha.
- Wachache wetu wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia Mfuko wa KAUKI na Mikutano Mikuu. Ombi letu ni kuwahamasisha wengine nao wachangie Mfuko wa KAUKI na hususani Mkutano Mkuu wa Tisa wa KAUKI, ambapo kwa mwaka huu utafanya uchaguzi wa viongozi na pia kuzindua ofisi yake Kidamali kama mipango ya ujenzi itaenda vizuri kama ilivyokubalika katika Mkutano Mkuu wa 8 wa KAUKI uliofanyika Jijini Dar es Salaam, mwezi Juni 2012.
- Fanikio jingine muhimu ni kufanikiwa kutengeneza Muundo wa Ukoo (Clan Structure) yenye kurasa karibu ya 80. Kila mwana KAUKI atapata nakala yake Wakati wa Mkutano Mkuu wa 9 wa KAUKI itakayofanyika Kijijini Kidamali. Inaonesha toka kizazi hiki kilipoanza hadi sasa…, pamoja na taarifa mbalimbali kuhusiana na Kabila la Wahehe zitatolewa.
Hima tunawaomba ndugu, jamaa na
marafiki wenye moyo wa kweli wa kuisaidia jamii inayotahidi kujisaidia kutuunga
mkono katika mchakato huu. Mfuko wa KAUKI una malengo mengi, ripoti zilizomo
kwenye blogu zinaeleza vizuri. Lakini pia unaweza kuwasiliana na viongozi wa
KAUKI kupitia anuani yao: tagumtwa-kauki@gmail.com au tagumtwa@gmail.com
na simu 0713 270364
Kwa taarifa mbalimbali unaweza
kuzipata kupitia blogu http://www.tagumtwa.blogoak.com
Imeandaliwa
na kutolewa kwa niaba ya uongozi na:
Adam Alphonce Sigatambule
Tavimyenda Tagumtwa Kivenule
KATIBU KAUKI
No comments:
Post a Comment