Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla

Mchakato wa Kuandaa Kitabu cha Chimbuko, Muundo na Historia ya Ukoo wa Kivenule na Uhehe kwa Ujumla
Karibu uone yale ambayo KAUKI inafanya

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014

Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI, 2014
Chimbuko na Muundo wa Ukoo wa Kivenule (2005 - 2009)

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI

Mkutano Mkuu wa10 wa KAUKI
Tangazo la Mkutano Mkuu wa 10 wa KAUKI

Tuesday, 15 January 2013

BANDARI SALAMA



JIJI LA MARAHA, DAR ES SALAAM

Dar es Salaam kama inavyotambulika toka enzi hizo kuwa ni Bandari ya Salama. Pengine wenzetu walikuwa na sababu za msingi kuiita hivyo. Kuna mambo mengi yalichangia ikaitwa Bandari ya Salama. Mojawapo ilikuwa ni mandhari mazuri na masafi ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi hicho. Pili ni kuwa katika mwambao wa Bahari ya Hindi, ambapo upepo mwanana safi uvumao toka Baharini ulikuwa unaifikia Pwani ya Dar es Salaam.

Suala jingine lilikuwa ni mpangilio mzuri wa majengo (majumba), barabara, bustani za maua na hifadhi za maeneo ya wazi na idadi sahihi wa watu. Pengine leo hii ukiwaalika hao watu waliipa hadhi ya Bandari ya Salama Jiji la Dar es Salaam, wanaweza kukataa kabisa.

Kuna sababu nyingi lakini kubwa ni uchafu uliokithiri ndani ya Jijini hili, unaoambatana na uozo unaonuka mithili ya mzoga; msongamano usioisha wa watu, magari, maduka na majengo. Kukosekana kwa usafiri wa uhakika na salama ambao unasetiri hadhi na heshima ya watumia vyombo hivyo vya usafiri; lakini pia hata matumizi ya lugha chafu ambayo yamezagaa kila kona bila kutofautisha baina ya mkubwa au mdogo. 

Hivi karibuni nilijaribu kutembelea maeneo ya Ubungo River Side na wakati napita pembezoni mwa barabara ya Mandela ambayo hupitisha magari makubwa na madogo, daladala na mabasi ya kwenda mikoa ya kusini; niliona mambo kadha wa kadha. Mengine yalikuwa mazuri kwani niliona maendeleo yamefanyika kwa kiwango kikubwa ikiwemo lile la ujenzi wa barabara bora ya Mandela na pia majengo kama Hoteli na Kumbi za Kisasa. 

Kwa bahati mbaya pamoja na uzuri ambao nimeuelezea, barabara hiyo nzuri pia inakumbwa na kasoro kubwa ya uchafu wa mitoro yake. Mitoro hiyo ina maji taka toka vyooni. Pia, inatoa harufu mbaya kwa yeyote anayetumia njia hiyo. Haijalishi upo ndani ya gari au nje ya gari. Watawala, viongozi, askari, watoto na wapenda maendeleo wanapita humo, lakini hata mmoja anayejaribu kukemea tabia ya uchafu huu hajajitokezeza.  

Zifuatazo ni picha zinazoonesha uhalisi wa mazingira hayo ya Ubungo River Side, Jijini, Dar es Salaam.






Mtaro wa Pembeni ya Barabara ukiwa usongwa na maji yenye Kinyesi. Jiulize, haya maji yanaelekea wapi? Bondeni ambapo mbeleni huko yanatumika kumwagilia mchicha?!!! 







































Sio maji kidogo au uchafu kidogo uliosongamana ndani ya mfereji huu, nenda jionee mwenyewe. usisubiri kuambiwa.





Maendeleo na uchafu, je tutafanikiwa? Juu barabara safi na magari na majengo ya kuvutia. Lakini ndani ya mtaro ni Kinyesi. Hii ndiyo Bongo Dar es Salaam






 Ukiangalia hapa, huwezi kuamini kama kwenye mitaro kumejaa kinyesi ambacho kinaharibu kabisa hewa ya maeneo haya ya barabara.
 





No comments:

Post a Comment